Gamboshi, ‘makao makuu ya uchawi na wachawi’ lakini wengi hawajui ilipo
Gari linalokokotwa na ng'ombe katika
barabara ya kuelekea kijijini Gamboshi. PICHA ZOTE|MIGUEL; SULEYMAN
Na Miguel Suleyman,
Bariadi (email the
author)
USIKU YAONEKANA KAMA JIJI LA NEW
YORK AU LONDON. WENYEWE WAMWOMBA RAIS KIKWETE, MZEE WA VIJISENTI AKAWASAFISHE
Gamboshi.Wakazi wa Kijiji cha Gamboshi,
kilichopo wilayani Bariadi, Mkoa wa Shinyanga, wamemuomba Rais Jakaya Kikwete
awasaidie kusafisha kijiji chao kutokana na jina baya lililoenezwa duniani
kwamba hapo ni makao makuu ya maovu ya uchawi ulioshindikana.
Kijiji hicho ambacho ni nadra sana kutembelewa, kimepata umaaurufu mkubwa ndani na nje ya nchi kikielezwa kuwa ni kitovu cha uchawi na wachawi wanaoweza kufanya miujuza, hali ambayo imekifanya kijiji hicho kupitwa na mkondo wa kimaendeleo.

“Sisi ni wakulima wakarimu wa pamba,
mahindi na mpunga. Yote mnayoyasikia kwamba sisi ni magwiji wa uchawi ni uvumi
uliotiwa chumvi nyingi. Tunamwomba Rais wetu kwa kushirikiana na Mbunge wetu,
Andrew Chenge watusadie kulisafisha jina letu,”alisihi Zephania Maduhu,
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Gamboshi.
Maduhu pamoja na wanakijiji wenzake
walidai kuwa, hofu iliyoenezwa ndani na nje ya nchi kuhusua uchawi uliovuka
mipaka wa Kijiji cha Gamboshi umesababisha madhara makubwa kwa kijiji chao
kiasi chakutengwa na jamii yote ya Watanzania.
“Hakuna aliyetembelea kijiji hiki
kwa miaka mingi sana. Hata sisi tunapotoka nje ya kijiji, wengi hawataki
kutusogelea wakiamini tutawadhuru, ” alisema Musa Deus (26), mmoja wa
wakulima walionufaika kilimo cha mkataba kijijini Gamboshi.
Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, tangu Uhuru mwaka 1961, hakuna kiongozi yoyote wakitaifa aliyewahi kukanyaga kijijini hapo.
Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, tangu Uhuru mwaka 1961, hakuna kiongozi yoyote wakitaifa aliyewahi kukanyaga kijijini hapo.
Anaongeza kuwa mtu wa pekee
aliyewahi kuzuru kijijini hapo ni mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge,
aliyefika kijijini hapo mwaka 2010, wakati akifanya kampeni za ubunge.
“Tume ya Katiba ilitupita, mwenge wa
Uhuru nao haujawahi kupita hapa.Tuko kisiwani mbali na Watanzania wengine,”
anasema Maduhu.
Kikiwa mafichoni kabisa, kiasi cha
kilometa 44 kutoka mjini Bariadi, Kijiji cha Gamboshi si rafiki wa watu wa
Kanda ya Ziwa kama ambavyo Mwananchi Jumapili ilibaini katika utafiti wake wa
muda mrefu.
Mijini na vijijini, kumekwepo na
ubishani mkali kuhusu ni mkoa gani unaokimiliki kijiji hicho, ambacho baadhi ya
wakazi wake wanadai kuwa miongoni mwa vioja vyake ni mauzauza yanayoweza
kuifanya Gamboshi ionekane kama Jiji la New York, Marekani au London, Uingereza
wakati wa usiku.
Pamoja na umaarufu wake, bado uwepo
wa Gamboshi umekuwa ni kitendawili kikubwa kwa jamii ya Wasukuma kutoka mikoa
ya Mwanza, Shinyanga na Simiyu.
Mbali na ubishani mkali kuhusu
kuhusu mahali hasa kilipo kijiji hicho cha miujiza, wengi wamekuwa wakidai
wakazi wake siyo jamii ya Kisukuma.
Wakazi wa Shinyanga wanadai kuwa
Gamboshi iko wilayani Magu, Mkoa wa Mwanza, wakati wale Mwanza wakidai kuwa iko
mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa Maduhu, Gamboshi iko katika Wilaya Bariadi, karibu na mpaka unaotenganisha na Wilaya ya Magu iliyoko mkoani Mwanza.
Kwa mujibu wa Maduhu, Gamboshi iko katika Wilaya Bariadi, karibu na mpaka unaotenganisha na Wilaya ya Magu iliyoko mkoani Mwanza.
“Tunaomba sana ndugu mwandishi,
waambie Watanzania kuwa mengi wanayoyasikia kuhusu Gamboshi siyo kweli kabisa.
Tunawakaribisha wote waje hapa kufanya biashara na sisi, waoleane na vijana wa
Gamboshi kama wafanyavyo katika vijiji vingine. Sisi ni binadamu wema,” anasema
mkazi wa kijiji hicho, Malimi Kidimi ambaye ni mkulima.
Ofisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Pamba(TCB), Ramadhani Dissa, anaielezea Gamboshi kuwa ni moja ya vijiji vilivyouza pamba nyingi msimu huu.
Ofisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Pamba(TCB), Ramadhani Dissa, anaielezea Gamboshi kuwa ni moja ya vijiji vilivyouza pamba nyingi msimu huu.
No comments:
Post a Comment